Our Vision and Mission Dira na Dhima Yetu
VISION DIRA
To be the most efficient Authority in the provision of water supply and sanitation services.
Kuwa Mamlaka yenye ufanisi zaidi katika utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira.
MISSION DHIMA
To provide affordable, reliable, and quality water supply and sanitation services that meet customer satisfaction.
Kutoa huduma bora, nafuu na za kuaminika za majisafi na usafi wa mazingira zinazokidhi matarajio na kuridhisha wateja.
Our Core Values Maadili Yetu
In day-to-day operations, KUWASA staff are guided by the following core values:
Katika utekelezaji wa shughuli za kila siku, watumishi wa KUWASA wanaongozwa na maadili yafuatayo:
Integrity Uaminifu
We commit to act honestly, fairly and openly, to honour our commitments and not use public office for personal gain.
Tunajitolea kutenda kwa uaminifu, haki na uwazi, kuheshimu ahadi zetu na kutotumia ofisi ya umma kwa manufaa binafsi.
Respect Heshima
We are committed to treating each other and the general public with respect by ensuring fairness, upholding merit principles and avoiding discrimination in office affairs.
Tumejizatiti kutendeana na kuwahudumia wananchi kwa heshima kwa kuhakikisha haki, kuzingatia misingi ya sifa na kuepuka ubaguzi katika utekelezaji wa majukumu ya ofisi.
Objectivity Usawa na Kutopendelea
We commit to act impartially in executing our duties and to provide the Government with objective and honest advice.
Tunajitolea kutenda bila upendeleo katika utekelezaji wa majukumu yetu na kuipatia Serikali ushauri wa kweli, wa haki na usio na upendeleo.
Excellence Ubora
We strive for excellence and work to the best of our abilities with pride, skill and dedication to provide timely, competent, fair, efficient and effective public service professionally and lawfully.
Tunajitahidi kufikia viwango vya juu vya utendaji na kufanya kazi kwa uwezo wetu wote kwa fahari, weledi, kujituma na dhamira ya kutoa huduma kwa umma kwa wakati, kwa umahiri, haki, ufanisi na ufanifu kwa kuzingatia misingi ya taaluma na sheria.
Creativity Ubunifu
We support continuous learning and encourage creativity and innovation to improve staff knowledge and skills and enhance services provided to KUWASA stakeholders.
Tunaunga mkono ujifunzaji endelevu na kuhamasisha ubunifu na uvumbuzi ili kuongeza maarifa na ujuzi wa watumishi wote na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wadau wa KUWASA.
Teamwork Kazi ya Pamoja
We believe in teamwork and participatory management, and we are committed to promoting citizen-centred service by collaborating with stakeholders to achieve KUWASA goals.
Tunaamini katika kazi ya pamoja na usimamizi shirikishi, na tumejizatiti kukuza huduma zinazomlenga mwananchi kwa kushirikiana na wadau katika kufikia malengo ya KUWASA.